top of page

Antibiotic ya kuua vimelea sugu yangunduliwa

 


Dawa mpya iliopewa jina la zosurabalpin, ilifanya kazi “vizuri sana” katika maabara na panya, alisema mkurugenzi wa kisayansi wa Ushirikiano wa Utafiti na Maendeleo ya Antibiotiki Ulimwenguni Prof Laura Piddock. Watafiti wa Marekani walilenga kupata njia mpya ya kutibu maambukizo yanayosababishwa na bakteria ya Acinetobacter baumannii (Crab) inayostahimili au yenye usugu dhidi ya carbapenem.


Kiumbe hicho, kilichopewa daraja la "priority-one critical pathogen" na Shirika la Afya Ulimwenguni, linaweza kusababisha maambukizo makali ya damu na kifua kwa wagonjwa mahututi wa hospitali. Inastahimili antibiotiki nyingi zinazojulikana.


Maambukizo yanayostahimili dawa yanaua mamilioni Na takribani 40-60% ya wale walioambukizwa hufa.


Sababu kuu ni ngumu kupata dawa mpya zinazoua ni kwa sababu ya muundo mgumu wa bakteria - na “membrane” yenye ukuta mara mbili inayozunguka na kuihifadhi dhidi ya shambulio. Muundo huu “unafanya iwe ngumu sana kupata dawa ndani yake na kupata dawa kubaki ndani”, alisema Prof Piddock alipofanya mahojiano na BBC.


Lakini zosurabalpin, iliyopatikana baada ya kupima takriban molekuli ndogo 45,000 zenye sifa za antibiotiki, inaonekana kuharibu uwezo wa kiumbe hicho kujenga kwa mafanikio membrane hii muhimu ya kinga.

 

MUHIMU

Dawacheck sio hospitali maelezo tunayotoa kwa muhtasari ni kwa ajili ya elimu na taarifa pekee na hayatakiwi kutumika kama mbadala wa ushauri wa daktari wako katika kituo cha afya


Taarifa bora, Afya bora ∣ Dawacheck®




bottom of page