top of page

Kwa nini kunywa pombe nyingi kwa wakati mmoja ni hatari zaidi kwa ini lako kuliko kunywa pombe kidogo kidogo kila siku

 


  • Watafiti wanasema kunywa pombe nyingi kwa wakati mmoja pamoja na hatari ya kijenetiki kunaweza kuongeza sana hatari ya kupata ugonjwa wa ini unaohusiana na pombe.

  • Wanaongeza kwamba, kuwa na ugonjwa wa kisukari aina ya 2 kunaweka watu wanaokunywa pombe nyingi katika hatari kubwa zaidi.

  • Wataalam wanasema matokeo ya utafiti yanaweza kusaidia kutambua watu wanaohitaji kulengwa na kupatiwa tiba kuzuia ugonjwa wa ini


Ugonjwa wa ini unaohusiana na pombe mara nyingi hufikiriwa kama ugonjwa unaohusiana na matumizi mabaya ya pombe ya muda mrefu, lakini utafiti mpya unaripoti kuwa ugonjwa huu mbaya wa ini pia unaweza kusababishwa na kunywa pombe nyingi kwa wakati mmoja (ulevi). Watafiti walisema kuwa watu wanaokunywa pombe nyingi kwa wakati mmoja na pia wana muundo wa kijenetiki unaowaweka katika hatari kubwa ya ugonjwa wa ini unaosababishwa na pombe wanaweza kuwa na hatari ya kupata ugonjwa wa ini mara sita zaidi ikilinganishwa na washiriki wa utafiti ambao waliripoti kunywa kidogo kidogo kila siku na walikuwa na uwezekano mdogo wa kijenetiki wa ugonjwa wa ini unaohusiana na pombe.


Watafiti walibainisha kuwa hatari hii ilikuwa kubwa zaidi miongoni mwa wale wanaokunywa pombe nyingi kwa wakati mmoja ambao pia walikuwa na ugonjwa wa kisukari aina ya 2.


Matokeo yao yalifafanuliwa katika utafiti uliochapishwa katika jarida la Nature Communications. Mtindo wa kunywa una mchango mkubwa zaidi katika kupata ugonjwa wa ini kuliko kiasi cha kunywa, walisema watafiti kutoka Chuo Kikuu cha London, Hospitali ya Royal Free, Chuo Kikuu cha Oxford, na Chuo Kikuu cha Cambridge.


“Wengi wa tafiti zinazochunguza uhusiano kati ya ugonjwa wa ini na pombe huzingatia kiasi cha pombe kilichotumiwa,” alisema Linda Ng Fat, mwandishi wa kwanza wa utafiti na mtafiti mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha London, katika taarifa kwa waandishi wa habari. “Tulitumia njia tofauti kwa kuzingatia mtindo wa kunywa na tukagundua kuwa hii ilikuwa kiashiria bora zaidi cha hatari ya ugonjwa wa ini kuliko kiasi peke yake. Matokeo mengine ya msingi ya utafiti huu yalionyesha kuwa vihatarishi vikiongezeka kuna hatari kubwa zaidi ya ‘ziada’ kutokana na mwingiliano wa vihatarishi hivyo.”


“Utafiti huu ni muhimu kwa sababu unaonyesha kuwa sio tu kiasi gani unakunywa kwa jumla lakini mtindo wa kunywa una umuhimu pia,” aliongeza Pamela Healy, afisa mtendaji mkuu wa British Liver Trust. “Kunywa kiwango kikubwa, haraka, au kunywa ili kulewa, kunaweza kuwa na matokeo mabaya kwa afya yako ya ini.”


Jinsi unywaji wa pombe unavyoharibu ini


"Mshtuko wa kunywa pombe unaweza kuzidi uwezo wa ini kumeng’enya pombe” na unaweza “kuathiri kwa ukali uwezo wa seli za ini kuishi kwa sababu ya uharibifu mkali."— Dr. Theodore Strange


"Unywaji wa pombe unaweka shinikizo kubwa kwenye ini, ambalo huwajibika kumeng’enya pombe. Wakati pombe inatumika kwa wingi, ini haliwezi kufanya mchakato wa kusafisha, hii husababisha mkusanyiko wa sumu na kupelekea ugonjwa wa ini baada ya muda."— Adam Zagha


Taasisi ya Kitaifa ya Matumizi Mabaya ya Pombe na Ulevi (NIAAA) Hufafanua ulevi kama vipindi ambapo mkusanyiko wa pombe kwenye damu (BAC) unaongezeka hadi 0.08% au zaidi. Kwa wanaume, inamaanisha kunywa vinywaji vitano au zaidi ndani ya saa mbili. Kwa wanawake, BAC hufikiwa kwa kunywa vinywaji vinne au zaidi katika kipindi kile kile.





Watafiti walisema kuwa ugonjwa wa ini ni miongoni mwa sababu kuu za vifo vya mapema ulimwenguni na inakadiriwa kuwa 2% hadi 3% ya idadi ya watu ulimwenguni wana ugonjwa unaopelekea kupata makovu kwenye ini (Cirrhosis) au ugonjwa wa ini (Liver Disease)


“Ni muhimu kwa watu wenye historia ya familia ya ugonjwa wa ini au wale walio na uwezekano wa kijenetiki wa kuwa walevi kujua hatari kubwa inayowakabili,” alisema Zagha. “Ujuzi huu unaweza kuwawezesha watu kufanya maamuzi sahihi kuhusu matumizi yao ya pombe na kutafuta msaada kabla ya uharibifu wa ini usioweza kurekebishwa kutokea.”


 

Taarifa bora, Afya boraDawacheck®



bottom of page